Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Israel wa Ben-Gurion ulifungwa kwa saa mbili Jumatatu asubuhi kama sehemu ya mgomo wa jumla wa kuishinikiza serikali kutia saini usitishaji vita wa Gaza ambao utawaachia huru mateka wa Israel.
Haya yanajiri baada ya mamia kwa maelfu ya waandamanaji kujitokeza mabarabarani kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza kufuatia kuokolewa kwa miili sita ya mateka kutoka katika eneo hilo lenye vita.
Umati wa watu unaokadiriwa na vyombo vya habari vya Israel kufikia 500,000 waliandamana mjini Jerusalem, Tel Aviv na miji mingine, wakitaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu afanye zaidi kuwarudisha nyumbani mateka 101 waliosalia, karibu theluthi moja kati yao ambao maafisa wa Israel wanakadiria kuwa wamefariki.
Chama cha wafanyakazi The Histadrut, ambacho kinawakilisha takriban wafanyakazi 800,000, kilisema kinalenga kuzima au kuvuruga sekta kuu za uchumi, zikiwemo benki, huduma za afya na uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo, ili kuweka shinikizo kwa serikali ya Israel.
Maelfu ya watu, baadhi yao wakilia, walikusanyika Jumapili usiku nje ya ofisi ya Bw Netanyahu mjini Jerusalem huku jamaa za mateka Tel Aviv wakiandamana wakiwa na majeneza kuashiria ushuru huo.
Jukwaa la Familia za mateka lilisema kifo cha mateka sita ni matokeo ya moja kwa moja ya Netanyahu kushindwa kupata makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwarudisha wapendwa wao nyumbani.
Ofisi ya Netanyahu ilisema kuwa imezungumza na familia ya Alexander Lobanov, ambaye mwili wake ulikuwa miongoni mwa waliopatikana, na kuomba msamaha na kueleza “huzuni kubwa”.
Lakini familia ya mateka mwingine, ilisema wamekataa kuzungumza na Bw Netanyahu, na badala yake wakawataka Waisraeli wajiunge na maandamano.
Waisraeli wengi wanamlaumu Bw Netanyahu kwa kushindwa kuwarejesha mateka wakiwa hai katika makubaliano na Hamas kumaliza vita vilivyodumu kwa miezi 10 Mazungumzo juu ya mpango kama huo bado yameendelea kwa miezi kadhaa.