Mkongwe wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi ambae kwa sasa baada ya kurejea katika kikosi cha Simba amerudishiwa majukumu yake ya zamani kama nahodha wa timu hiyo na Hassan Is-Haka kuwa nahodha msaidizi, August 12 Mgosi anatupa utofauti kuhusiana na Simba ya sasa na alioiacha.
Mgosi ambae anaichezea klabu ya Simba kwa awamu ya pili toka alivyoondoka mwaka 2011 kwenda DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, sasa amerudi katika Simba tofauti kidogo na aliyoiacha kwani sasa kuna wachezaji wengi vijana na wengine huenda walimsikia Mgosi akiwa toka wapo Shuleni.
“Kuna utofauti mkubwa kwani wachezaji wa sasahivi na waliokuwa nyuma ni tofauti… kipindi wanacheza wakina Matola, Pawassa na vijana waliokuwepo sasahivi kuna utofauti mkubwa. Mwisho wa siku Simba inabaki kuwa vilevile, heshima ni kubwa kwangu na sijaenda nao tofauti sana… heshima ipo hadi wananiita Uncle maana ni kaka wa mama au mdogo wa mama”>>>Mgosi
Sauti ya Mgosi kwenye exclusive na millardayo.com unaweza kuisikiliza hapa mtu wangu ukibonyeza play.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos