July 12 2016 Geah Habib alituletea hekaheka kutokea Tandale hospitali iliyokuwa ikimuhusu mgonjwa aliyetoka nje ya hospitali na kukaa nje ya hospitali na akalala nje usiku kucha, na mashuhuda siku hiyo walisema hospitali walipopewa taarifa hawakujali. Mashuhuda walidai kuwa alishindwa kuhudumiwa kwa sababu alikuwa hana shilingi 2000 ya kadi na mpaka anakata roho alikuwa nje ya hosptali hiyo.
Sasa leo July 18 2016 kupitia hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea mwendelezo wa hekaheka baada ya kuwapata ndugu zake na Mganga mkuu wa wilaya ambapo wameelezea ishu nzima ilivyokuwa, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye HekaHeka ya leo.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Aziz Msuya amesema……..>>>’baada ya kuonana na madaktari walimshauri kumpa dawa alikataa alikuwa na mwenza wake na wote wawili walikuwa wamelewa, madaktari dawa ambazo walitaka kumpa ni zile ambazo haziwezi kumdhuru hata kama alikuwa amelewa lakini kwa bahati mbaya alikataa’
>>>baada ya kukataa kutibiwa pale walipewa barua ya rufaa yeye na mwenza wake wakatoka nje ya geti wakawa wanasubiri usafiri, tungeweza kumpeleka na ambulance lakini ilikuwa service, mwenzake alimuacha pale nafikiri alimuambia amsubiri mwenzake ili waweze kwenda hospitali’:- Aziz Msuya
Kuisikiliza full story, bonyeza play hapa chini
ULIKOSA HII KWA MARA YA KWANZA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUWEKA BETRI KWENYE MOYO WA MTOTO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI