Hatimaye barabara ya Keko imefanyiwa marekebisho ya awali na hii ni baada ya maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe kuwapa siku 7 Wakandarasi waliopewa tenda ya kujenga barabara ya Mwendokasi kufanya marekebisho ya awali ili barabara ipitike.
“Haya ni matengenezo ya muda mfupi hii barabara ipo kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi, Wakandarasi wamefanya uzembe ila wamefanyakazi, kazi yao wakati wanatengeneza barabara hii wanatakiwa wahakikishe magari yanapita, nimeona baada ya kutengenezwa barabara naona madereva wanaenda kasi sana tutaweka matuta” DC Gondwe