Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ‘alizamia’ kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikitokea Nairobi ameanguka na kufariki dunia dakika chache kabla ya ndege hiyo kutua Uwanja wa Ndege wa Heathrow mjini London.
Mwili huo ulipatikana katika bustani ya Clapham, haijafahamika mara moja kilichosababisha mtu huyo kudondoka toka kwenye ndege hiyo na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi.
Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua.
Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake.
Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa.
Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesema: “Ndege hii huchukua saa 8 na dakika 50 kukamilisha safari yake. Inasikitisha kuwa mtu alipoteza uhai wake baada ya kuingia ndege yetu kisiri”