Wananchi katika kijiji cha Lugunga kata ya Lugunga Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa Fisi ambao wamekuwa wakijisaidia katika Machinjio ya kijiji hicho hali ambayo imekuwa ikiwakela huku wakiiomba Serikali ya Kijiji hicho kuchukua hatua.
Akiwasilisha Changamoto hiyo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Bw. Charles Yusufu Mkazi wa Kijiji cha Lugunga amesemamara nyingi wanapokuwa wanatumia Machinjio hiyo wamekuwa wakikuta vinyesi vya Fisi katika Machinjio hiyo huku akisema Machinjio hiyo inategemewa kulisha Vijiji zaidi ya sita ndani ya kata hiyo.
“Tunayo Machinjio kwakweli Machinjio usiku wanaenda kujisaidia Fisi ahsubuhi tunaenda kuchinjia machinjio sio rafiki tulitamani kipindi unapasha ungeingilia chocho hapo kusudi ukaone uje uzungumzie tunayo machinjio yanayolisha vijiji visiyopungua Sita , ” Charles Yusuph Mkazi wa kijiji cha Lugunga.
Katika hatua nyingine wananchi wameimba serikali kutatua Mpaka wa soko la Lugunga mpaka wa Kijiji cha Luhara ambao umekuwa na Changamoto ya Soko la Kijiji cha Lugunga kuhamishiwa katika Kijiji cha Luhara huku wakiwaomba wataalamu kufika na kutatua Sintofahamu hiyo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Lugunga amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akisema tayari wamekwisha kukusanya Mifuko 12 ya Saruji kwa ajili ya Ukarabati wa Machinjio hiyo .
Naye Mbunge wa Jimbo la Mbogwe ,Nikodemas Maganga amewataka Viongozi wa Serikali kutatua changamoto ya Machinjio pamoja na Mipaka katika soko hilo ambalo limekuwa likileta utata wa yupi mmiliki sahihi huku wananchi wa kijiji cha Lugunga wakiomba Mh Mbunge kulitaftia ufumbuzi suala hilo.