Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi William Lukuvi January 27, 2018 amefika Ofisi za Manispaa ya Ilemela Mwanza na kuamua kufanya ukagazi yeye mwenyewe kwenye mafaili ya watu ambao hawajapatiwa hati ya zao.
Katika ukaguzi huo Lukuvi alikuta mapungufu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mafaili kutopitiwa na Maafisa ardhi na wengine kutojibiwa kwa wakati kitu kinachosababisha baadhi ya watu nyumba zao kuuzwa.
“Huu uzembe unatoa tafsiri kwamba huduma kwa wananchi ni sifuri, sababu amjibu barua zao wala kusoma barua wanapoandika, wakuu wa idara msome, unaweza kuta kuna watu hawaja hudumiwa zaidi ya miaka ya 20,”-Lukuvi
DR. MWIGULU NCHEMBA NA WASIRA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM KINONDONI