Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amesema anatarajia kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM leo Jumamosi Agosti 11,2018.
“Nimejiridhisha kwa hitaji la Nafsi yangu kwamba nijiunge na Chama cha Mapinduzi CCM, nawajulisha watanzania rasmi kuwa nimeanza mipango ya kutekeleza hili mara moja”- Julius Mtatiro.
“Mimi sasa siyo mwanachama wa CUF tena nimejivua nyadhifa zangu zote, sasa naanza kutumia uwezo wangu wote Nitaanza kufanya siasa za vitendo kwa kumshauri Rais kujenga nchi yangu”.
“Kuna vijana wadogo tu wamefanya mambo makubwa kwa kuwa wako katika majukwaa sahihi nimetafakali Sana nimeona ni achane na siasa za ubabaishaji siasa za ushabiki” Julius Mtatiro.
Amesema ameshamwandikia Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF, kuhusu msimo wakekuhusu kuachana na Chama hicho, na sasa amefanya maamuzi ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
HISTORIA: Alivyopata jina Majuto | Kuacha Jeshi | Rekodi anayoshikilia | Umauti