Leo June 8, 2018 stori ninayokusogezea ni kutoka upande wa soka ambapo Serikali ya Ghana imevunja Chama cha Soka nchini humo baada ya rais wa Chama hicho, Kwesi Nyantakyi kukamatwa akipokea rushwa.
Kwesi Nyantakyi amekamatwa akipokea $65,000 ambazo ni zaidi ya Tsh. Milioni 148 kutoka kwa Mwandishi habari mpelelezi aliyejifanya kuwa mfanyabiashara mwenye hamu kubwa ya kuwekeza katika soka nchini Ghana.
Mpaka sasa, Nyantakyi ambaye pia ni Afisa wa pili kwa uwezo katika soka la Afrika hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.
Waziri wa habari Mustapha Abdul-Hamid, amesema Serikali imekivunja chama cha soka Ghana GFA, kutokana na muozo ulionekana na hatua za muda za kuongoza soka zitatangazwa hivi karibuni
FULL STORY: Producer aeleza dakika za mwisho za maisha ya ‘SAM WA UKWELI’