Leo July 27, 2018 Taarifa nayokusogezea ni kutoka Bandari ya DSM ambapo Meli mpya ya kubebea magari iitwayo Morning Conductor Panama imetia nanga leo.
Kwa mujibu wa alicho-post Gerson Msingwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu meli hiyo ina uwezo wa kubeba Magari 2000 au Tani 57,542 za mizigo na inaendeshwa na Kampuni Eukor Car Carriers Inc ya Korea.
Bandari ya DSM imeandika rekodi ya juu kuwahi kutokea kwa kupokea Tani Milioni 16.2 katika mwaka 2017/2018.
LIVE MAGAZETI: ‘Bila Nape, Bashe CCM itakufa’, Lissu: Ukweli utajulikana, Siri nje