Bado naendelea kukusogezea stori kutoka bungeni ambapo moja ya headline iliyosikika ni pamoja na huu mpango wa serikali ya Tanzania kutangaza mpango wake wa kuanza kuwalipa pensheni wazee wote nchini wa kaunzia umri wa miaka 70 ambapo ambao unatarajia kuanza kutekelezwa hivi karibuni.
Akimjibu mbunge wa Magu Boniventura Kiswaga aliyehoji lini serikali itaanza lini kuwalipa kiinua mgongo wazee waliotumikia taifa Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Anthony Mavunde amesema…>>>’Kwa mujibu wa sheria kiinua mgongo ni malipo yanayolipwa na mwajiri kama asante baada ya kumaliza mkataba‘
‘Serikali inaandaa mpango wa pensheni kwa wazee nchini ambapo hadi sasa imeshatekeleza mambo kadhaa ikiwemo Kuanisha idadi ya wazee wote nchini, kuanisha viwango vya pensheni, kuandaa utaratibu wa kulipa pensheni hizo ikiwa ni pamoja na kusimamia, kuwashirikisha wadau kuandaa mpango huo‘ –Anthony Mavunde
Serikali imetangaza mpango wa kuanza kuwalipa kiinua mgongo wazee wote wa kuanzia umri wa miaka 70, kiwango cha mwanzo kitakuwa elfu 20
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
ULIMIS MANENO YA PROFESA TIBAIJUKA BAADA YA KWENDA KUSHUHUDIA TETEMEKO LA ARDHI