Kama ni Mfanyakazi unaye deal na mafaili au kama ni mteja ambaye umeshakutana na kero ya kaa kwanza zaidi ya robo saa mpaka siku ili wakutafutie faili basi mkombozi wa kero ameshapatikana.
Wanafunzi wa Chuo kikuu Salumu P. Salumu na wenzake wawili ameweza tengeneza kifaa ambacho kitasaidia mashirika na taasisi ambazo huwa na mafaili mengi ya wateja ambapo hupata tabu zaidi kutafuta mafaili hayo
Salumu anasema kifaa chake kinawezesha kufanyiwa kazi kwa faili lako ambapo kama umepeleka na halijafanyiwa kazi ndani siku saba hutoa taarifa kwa njia ya sms kuwa faili fulani halijafanyiwa kazi, pia kama unalitafuta hutoa mlio ambao unasaidia kuliona lilipo pia na kuonyesha mahali lilipo kupitia google Map.
Salumu anaeleza kuwa ni vigumu kwa wadukuzi wa mtandao kudukua mtandao huo kwasababu ya ulinzi walioweka ambao hauruhusu mtu kudukua taarifa katika mtandao huo.
MAJIBU YA IGP SIRRO BAADA YA KUULIZWA MO YUKO HAI AU AMEKUFA