Tatizo la foleni mahospitalini hukera zaidi watu hasa pale Mtu anapokuwa mgonjwa na kukuta watu wengi kwenye foleni ya kuingia kwa Daktari na muda wa kupima na wakati mwingine unaweza kuta hata vipimo kwa muda huo havifanyi kazi labda kwa tatizo la kutokuwepo kwa umeme (kukatika) au hata mpimaji kutokuwepo maabara au kuwa na kazi nyingi.
Mwanafunzi wa kitanzania Janeth Tillya kutoka Chuo cha St Joseph cha DSM ameweza kutengeneza kifaa ambacho mtu anaweza jipima matatizo ya moyo kisha kumtumia Daktari wake matokeo yake hata bila ya kwenda Hospitali kwa wakati huo ambao anajisikia vibaya.
Kifaa hicho ambacho kinatumia betri dogo la kawaida ambalo linapatikana katika maduka ya kawaida majumbani ndilo linatumika kuendeshea kifaa hicho ambacho pia kinatumia Bluetooth kutuma taarifa katika simu wakati unajipima.
Dereva pekee anaendesha gari la Nyerere la Mwaka 1954 (+video)