Leo July 8, 2019 Watu saba wakiwamo wafanyakazi watano Uongozi wa Azam Media Limited, wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga.
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8 asubuhi, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori wakati wafanyakazi hao wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi kesho Jumanne Julai 9.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando amethibitisha wafanyakazi waliofariki kuwa ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo, Charles Wandwi na dereva na utingo wake ambao majina yao hayajafahamika.
Wengine wawili waliojeruhiwa na wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde na Artus Masawe ambaye hali yake inadaiwa kuwa nzuri kiasi.
BIBI MZEE ALIEZUNGUSHWA ARDHI YAKE KWA MIAKA 12, RAIS MAGUFULI AMRUDISHIA