Leo September 6, 2018 Mbunge wa Serengeti kwa tiketi ya CHADEMA Marwa Ryoba amesema yupo tayari kuacha ubunge ili awape wananchi waliomchagua barabara ya lami.
Akizungumza katika ziara ya Rais John Magufuli wilayani Serengeti, Ryoba amesema wilaya hiyo haijanufaika na Hifadhi ya Serengeti kutokana na kukosekana kwa barabara ya lami.
“Mimi nipo tayari hata kuacha ubunge lakini unipe barabara, WanaCHADEMA wote sisi ni wa kwako, vyama vyote vya upinzani sisi ni wa kwako usitutupe Rais, tupo chini ya magoti yako” -Mbunge wa Serengeti Chacha Marwa akiongea mbele ya Rais Magufuli
Lugola “Rais Magufuli nakutafutia wateja wa Mahakama ya Mafisadi, ina uhaba”