Mwezi mmoja uliopita kama Taifa tulikua katika majonzi mazito baada ya ndugu zetu kufariki katika ajali ya kuzama kwa Kivuko cha Mv Nyerere katika wilaya ya Ukerewe mkoa wa wa Mwanza na zilisemwa sababu nyingi sana ambazo zilizosababisha mpaka kuzama kwa kivuko hicho.
AyoTV na millardayo.com imewapata wanafunzi wawili kutoka Chuo cha Bahari (DMI) cha Jijini DSM ambao wao wametengeneza boti ndogo ambayo itasaidia kwa wakazi ambao hupata shida kuvuka maji hasa wakati wa mafuriko na wanaoishi katika mito mikubwa na hawana vivuko.
Wanafunzi hao wana idea yao watakayoweka katika kivuko hicho ambapo wanasema wataweka kifaa kama boti imepakia mzigo mkubwa zaidi kupita uwezo wake injini za boti hazitawaka kabisa, na kama nahodha wa boti hizo akiingia amelewa pia haitaweza kuondoka na itapiga Alarm.
Soggy Doggy “Kila mtu anataka kuwa Diamond Platnumz” (+video)