Leo June 23, 2018 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amenusurika baada ya mlipuko kutokea katika mkutano aliokuwa anahutubia katika eneo la Bulawayo.
Video kutoka katika uwanja wa michezo wa White City inaonesha Mnangagwa akiondoka kwenye jukwaa baada ya kutoa hotuba, mlipuko unapotokea.
Msemaji wake amesema rais huyo hajajeruhiwa. Baadhi ya watu wamejeruhiwa. Msemaji wa rais George Charamba ametoa taarifa akisema “Kumekuwa na majaribio kadha ya kumuua rais miaka mitano iliyopita.”
Gazeti la serikali la Herald limeripoti kuwa Makamu wa rais Kembo Mohadi ameumia miguuni wakati wa mlipuko huo unaodhaniwa kutokana na bomu, lakini taarifa hizo hazijathibitishwa.
MAGAZETI LIVE: Maiti tano zadaiwa kuzikwa kanisani, TRA kupiga mnada makontena ya vigogo