Leo September 29, 2018 Rais Dkt John Pombe Magufuli ameeleza sababu ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suzan Kolimba ni kuwa kiongozi huyo alishindwa kuwasimamia Wakurugenzi ndani ya Wizara hiyo.
Rais Magufuli amesema wizara hiyo imekuwa haimridhishi kwa namna ambavyo Naibu Waziri aliyepita badala ya kuwasimamia wakurugenzi wa wizara na kusema yeye ndio alikuwa akisimamiwa na watendaji wake.
Rais Magufuli “siku nyingi wizara mambo ya nje haijanifurahisha sana mambo yake mengi hayaendi vizuri, Wakurugenzi wake wengi ni dhaifu sana, wizara ile viongozi wake wanatembea sana, sio unakuwa na Naibu Waziri anayeendeshwa na Wakurugenzi badala ya kuwaagiza unachotaka wewe yani wakuongoze, ndio maana niliamua kuwatoa wote Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake.”