Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.
Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani mara moja.
“Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani” RC Makonda.
Mbunge aliepiga magoti Jimboni, afunguka mafanikio ya Miaka Mitatu