Mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi Rais Magufuli.
Kalanga amepokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.
“Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa. Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu… Watu wa Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi,” Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.
Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia CHADEMA 2015.
LIVE MAGAZETI: Waliomdhalilisha Jokate ”watapata tabu sana”, “Nawasha moto kumchoma Mbowe”