Leo June 26, 2018 Jeshi la Polisi limetangaza kusitisha utoaji wa ajira zilizotangazwa kwa vijana wa JKT waliopita oparesheni Kikwete ambazo zilikuwa zimetangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Mussa Taibu leo akielekeza kwa wote ambao wameshatuma maombi na ambao wana nia ya kutuma.