Leo August 25, 2018 ninayo stori kutoka kwa Waziri Mstaafu wa muda mrefu katika awamu mbalimbali nchini Prof. Mark Mwandosya amaetoa funzo kupitia ukurasa wake wa Twitter hii ni baada ya mtu kumfuata na kumuomba hela ya ada kwa ajili ya Mwanae.
Prof. Mwandosya alipoombwa ada alijibu alikataa na kumtaka mwombaji aunde Kamati kama ambavyo huwa wanafanya kwenye harusi.
Nanukuu alichoandika Prof. Mwandosya “Rafiki ameniomba msaada. Kijana wake amepata nafasi chuo kikuu anahitaji ada. Nimemuuliza ingekuwaje kijana angekuwa anaoa? Kajibu wangeunda kamati. Nimeshauri wafanye, waorodheshe marafiki, mimi nikiwemo, ili kama ilivyo harusi tuchangie. Kusiwe na kuvunja kamati. Katika hili,Tubadilike.”
RAIS MAGUFULI AMTUMA MSTAAFU KIKWETE ZIMBABWE, CHEYO NAE