Leo June 30, 2018 kuna hii ya kuifahamu kuhusu Makampuni nchini China yanaripotiwa kufuatilia hisia za wafanyakazi kwa kutumia sensa ndogo zilizowekwa chini ya kofia maalum.
Kampuni hizo hutumia data zilizokusanywa kutoka kwenye kofia ili kutambua msongo wa mawazo(stress), sonona (depression), na masuala mengine ambayo yanaathiri utendaji wa wafanyakazi.
Ikiwa suala lolote limegunduliwa, mfanyakazi atapewa ruhusa ya kwenda kupumzika nyumbani au mtumishi huyo atahamishwa kufanya kazi katika idara nyingine ambako kazi si nyingi sana.
Hangzhou Zhongheng Electric ni moja ya makampuni mengi ambayo hutumia helmeti hizi. Na wanasema kuwa kifaa hiki kimebuniwa kuongeza ufanisi wa kazi kwa jumla. Wao wamethibitisha kuwa teknolojia hii ilifanya kampuni yao kuzalisha zaidi.Teknolojia hii imeongeza ukaribu zaidi kati ya wafanyakazi na waajiri wao.
MAGAZETI LIVE: Wabunge Serikali wavutana mpaka usiku, Mwanafunzi darasa la nne apata mimba