Leo June 27, 2018 Kuna hii ya kuifahamu kutoka katika Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo kwa kushirikiana na SportPesa imetangaza washindi wa kwanza wa promosheni ya mwezi mmoja ya Amsha amsha na Airtel Money na ushinde ambayo ilizinduliwa June 14 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari DSM leo wakati wa kutangaza washindi hao, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema kuwa droo ya kupata washindi hao imesimamiwa na kuchezesha kwa wazi na Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania ambayo ndio wenye jukumu la kusimamia michezo yote ya bahati nasibu hapa nchini.
“Kama mlivyoona hapa kwa siku ya leo, droo yetu imechezesha kwa uwazi na hii inaamanisha kila mteja anayo fursa ya kuwa mshindi” alisema Mmbando
“Kila mteja wa Airtel Money anachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha anabet siku ambayo droo iko wazi na moja kwa moja namba yake itaingizwa kwenye droo ya wiki. ” Mbando
“Mteja atatakiwa kubet siku ya droo ili kupata nafasi ya kuwa moja ya washindi,” alisema Nchuda huku akiongeza kuwa wateja wanatakiwa kuhahakikisha kuwa wanayo pesa kwenye akaunti yao ya SportPesa.
Mmbando amesema kuwa washindi wa leo kumi wamejishindia simu mpya za smartphone kila mmoja, wengine kumi wamejishindia jezi za timu za Simba na Yanga huku wengine kumi kila mmoja akijishindia tiketi ya kushuhudia mechi za Simba na Yanga kwa msimu wote wa 2018/2019.
Nae Meneja Uhusiani wa SportPesa Sabrina Msuya alisema kuwa tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya amsha amsha mwaka huu, droo imekuwa wazi kila siku kuanzia saa sita usiku mpaka 11:59 kwa siku inayofuata kwa muda wote wa promosheni na kila mteja anachotakiwa kufanya ni kubet siku ya droo na namba yake itaingizwa kwenye droo moja kwa moja.
LIVE: Staa wa ManCity/Swansea yupo DSM anaongea na waandishi wa habari