Imezoeleka kuona baadhi ya watu wenye mahitaji maalumu wakitembea barabarani au katika ofisi mbalimbali wakiomba msaada wa fedha au vitu mbalimbali kwa ajili ya kujikimu kimaisha hii ni kutokana na maisha duni ambayo wamekuwa wakiyakabili.
Hii imekuwa ni tofauti kwa Shabani Ramadhani Mkazi wa Mkoani Kigoma ambaye yeye ana ulemavu wa kuongea na kusikia yani ni bubu na pia ni kiziwi ambaye licha ya hali yake hiyo bado amekuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya familia yake kupitia shaughuli yake ya ukinyozi.
Shabani ana Mke na Mtoto mmoja anafanya shughuli yake ya ukinyozi ambayo mpaka sasa ni takribani miaka saba tangu alipoanza lakini cha kusikitisha ni kuwa hakuzaliwa akiwa na ulemavu wa kusikia ambao anasema kuwa ulemavu huo ulianza taratibu alipokuwa mtoto mdogo.