Jeshi la Polisi nchini Mexico limemuachia huru kiongozi wa kundi la dawa za kulevya kwenye mji wa Sinaloa baada ya kuzidiwa uwezo na vikosi vya kundi hilo.
Ovidio Guzmán (28) ambaye ni mtoto wa muuza dawa za kulevya maarufu duniani El Chapo aliachiwa huru baada ya mapigano makali yaliyohusisha silaha za moto kwenye mji wa Culiacán nchini Mexico.
Waziri wa ulinzi wa Mexico Alfonso Durazo amesema walifikia maamuzi ya kumuachia masaa machache baada ya kumkamata ili kuweza kunusuru wananchi mitaani waliokuwa hatarini kutokana na mapigano hayo.
Kukamatwa kwake kunakuja mwezi mmoja baada ya baba yake Joaquín “El Chapo” Guzmán kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa usambazaji wa dawa za kulevya na uhalifu.