Watumishi wa Halmashauri ya Jiji na Wilaya ya Mbeya wanaomiliki vibanda vya biashara katika maeneo mbalimbali Jiji la Mbeya wapo hatarini kufukuzwa kazi iwapo hawatafikisha taarifa zao kwa Mkurugenzi ifikapo Jumatatu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Mbeya Albert Chalamila wakati akizungumza na Watendaji wa Halmashauri hizo kufuatia watumishi hao kudaiwa kuhodhi vibanda vya biashara na kuwa kikwazo kwenye ulipaji wa kodi huku wakikodisha vibanda hivyo kwa gharama kubwa na kusababisha Halmashauri kukosa mapato.