Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema amepewa vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo wadogo 25000 ambavyo anatakiwa avigawe Mkoa mzima na kila mjasiriamali atakayepewa kitambulisho anatakiwa alipie Shilingi 20000/=.
RC Shigela ameyasema hayo wakati wa kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote zilizopo Mkoani Tanga na kuwaasa kusimamia vizuri zoezi hilo katika maeneo yao ya kazi bila upendeleo wowote na kuhakikisha walengwa wananufaika kama Rais alivyokusudia.
Aidha RC amesema kila pesa zitazoingia Wilayani si vyema kwa Mtendaji wa Serikali kuharibu mafuta kupeleka pesa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa bali ni vyema akaituma kwenye account ili kuepusha matumizi mkubwa ya fedha kwa mambo ambayo yanaweza kutatulika kirahisi.
AGIZO LA RAIS MAGUFULI LILIVYOFANYIWA KAZI NA JESHI LA MAGEREZA