Leo July 4, 2018 tunayo story kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Ngonyani “Majimarefu” ambapo ameagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuagwa mwili wake umesafirishwa kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi ambapo wabunge mbalimbali walizungumzia kifo chake.
Akizungumza kwa niaba ya Kambi rasmi ya upinzani Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR- Mageuzi) amesema kifo cha Majimarefu kitumike kama changamoto katika kuhakikisha usalama wa afya za wabunge na watanzania.
“Ndugu yetu Stephen Ngonyani mwaka jana alinishirikisha kuhusu ugonjwa wake, amepata tabu, huyu ni Mbunge wa 5 anaondoka tangu Bunge hili limeanza mwaka 2015,” -Mbatia
“Lakini kwenye ngazi ya ubunge tunatumiaje changamoto ya kifo cha ndugu yetu kuhakikisha afya zetu zinakuwa salama zaidi?, kwenye Bima yetu ya Afya namna gani tunakuwa na Universal Heath Care System ambayo itamfanya kila mtanzania awe na uhakika na maisha?” amesema Mbatia