Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Meryprisca Mahundi, amefanya ziara wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza sehemu ulipojengwa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Sota, na kusema kuwa huo ni miongoni mwa minara 758, ambayo Serikali imeweka nguvu kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya mawasiliano yenye uhakika.
Mhandisi. Mahundi amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kutapeli na kurusha picha zisizo na maadili kwani kwa watakao bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katika ziara hiyo, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi. Imelda Salum, amesema kuwa Wizara inaendelea na mchakato wa kushirikiana na Mfanyabishara mkubwa Duniani Elon Musk, kutoka nchini Marekani kuleta teknolojia ya intaneti yenye kasi inayotumia anga za juu, huku akieleza ushirikiano huo unalenga kuboresha zaidi mawasiliano nchini.