Naibu Waziri Mkuu na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Utamaduni na Sanaa utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024 ukishirikisha wadau takribani 800 wa Tanzania Bara.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari leo Februari 27,2024 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ameeleza kuwa mkutano huo ni katika kuendelea kuimarisha sekta za Utamaduni na Sanaa nchini lengo ikiwa ni kujadili kwa pamoja mwenendo wa sekta hizo pamoja na kuziboresha.
“Kupitia mkutano huo wadau wa Utamaduni na Sanaa watapata wasaa wa kujengewa uwezo ,kubadilishana uzoefu , kufahamiana, kuendesha mijadala yenye afya kwa ajili ya kubainisha changamoto zinazoikabiki Sekta na kuweka mikakati ya kuitatua pamoja na kuwatambua na kuwatunuku wadau waliofanya vizuri katika zekta hizo” ameongeza Katibu Mkuu Msigwa.