Leo July 23, 2018 Afisa Mchunguzi wa TRA, Tumaini Fadhir ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa mamlaka hiyo, Jennifer Mushi anayekabiliwa na kesi ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya Shilingi Milioni 197 aliajiriwa TRA na mali zake.
Afisa huyo ameyaeleza hayo wakati akiongozwa na wakili wa Jennifer, Fulgence Masawe kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Katika ushahidi wake, Fadhiri amedai yeye ni mchunguzi wa ndani wa TRA, huku majukumu yake ni kufanya uchunguzi wa malalamiko yote na kuhakiki mali za watumishi ili kudhibiti vitendo vya rushwa.
Fadhiri alipoulizwa na wakili Masawe kwamba anamfahamu Jennifer, alijibu kuwa anamfahamu kwa sababu aliwahi kumchunguza.
Pia aliulizwa kama anafamu idadi ya mali za Jennifer na thamani yake , Tumaini alijibu anafahamu.
Pia aliulizwa Jennifer alianza kazi lini TRA, alijibu kuwa tangu mwaka 2010, lakini awali aliajiriwa katika sekta binafsi.
Pia alipoulizwa kama Jennifer aliajiriwa TRA akiwa na mali zake, Fadhir alijibu ndio.
Pia alipoulizwa ametumia mfumo gani kubaini idadi ya magari ya Jennifer, amedai kuwa alitumia mfumo wa usajili wa magari lakini hajawahi kuyaona kwa macho.
Naye wakili wa serikali Peter Vitalis alimuuliza Fadhiri ni mali gani ambazo Jennifer anamiliki, amedai kuwa ni zaidi ya magari 10 na waliyabaini kwa sababu alishindwa kuorodhesha vitu hivyo.
Baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi August 16,2018.
Mushi anakabiliwa na kosa la kumiliki magari 19 ambayo anadaiwa aliyaingiza nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 197,601, 207.
BREAKING: Watu watano wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Bilionea Msuya