Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kufuatia vifo vya watu 26 vilivyotokea March 24, 2018 saa 3 usiku, baada ya basi dogo (Hiace) lililokuwa limebeba abiria kugongana na lori lililokuwa limebeba chumvi katika kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Rais Magufuli amemtaka Mhandisi Evarist Ndikilo kumfikishia salamu za pole kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo na pia amevitaka vyombo vinavyoshughulikia usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili.
“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo vya watu 26 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga Mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu kazi ya Taifa.” -JPM
“Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea” -JPM
Amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema na majeruhi 9 wa ajali hiyo wapone haraka ili waungane na familia na jamaa zao kuendelea na shughuli za kila siku.
Basi hilo lilikuwa linatoka Mkuranga kuelekea Kimanzichana wakati lori lilikuwa linatoka Lindi kuelekea Dar es Salaam.
BREAKING: AJALI YA LORI NA HIACE IMEUA WATU 26 PWANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA NA KUSIKILIZA