Wazazi wa Michael Rotondo mkazi wa New York Marekani wamemfikisha mahakamani mtoto wao huyo kwa kugoma kuhama nyumbani huku akiwa hasaidii chochote. Wazazi wao wamesema Michael amegoma kuhama na kutafuta kazi licha ya kuahidi kumpa fedha kuanzia maisha. Jaji ameamuru kuhama.
Nyaraka za mahakama zinasema kuwa Michael Ratondo mwenye miaka 30 halipi kodi ya nyumba wala hasaidii kazi za nyumbani na amepuuza msaada wa kifedha wa wazazi kutaka kumwezesha apate nyumba yake ya kuishi.
Ratondo ameandikiwa barua tano na wazazi wake wakimtaka ahame suala ambalo amelipuuza.
Ratondo amelalamikia kuwa hakupewa muda wa kutosha kumwezesha kuondoka.
Wazazi wake walipeleka kesi kwenye mahakama ya Onondaga karibu na Syracue, New York tarehe saba mwezi May baada ya miezi kadhaa ya jitihada za kumshawishi mtoto huyo kuhama kufeli.
“Kuna ajira nyingi hata kwa wale walio na historia mbaya ya kazi kama wewe, Tafuta moja ni lazima ufanye kazi!” walisema Wazazi wake
Mahakama ilijibu na kusema kuwa Ratondo, ni mmoja wa watu wa familia na watahitaji uamuzi wa mahakama ya juu zaidi kuweza kumhamisha.
Sasa familia hiyo ya Rotondo itapeleka kesi yao kwenye mahakama ya juu baadaye wiki hii siku chache kabla ya yeye kufikisha umri wa miaka 31.