Rais wa Zimbabwe Emmerson Dambudzo Mnangagwa, June 28, 2018 aliingia nchini ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli na pia walifanya mazungumzo ikulu jijini DSM na kuafikiana kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Baada ya mazungumzo kumalizika Rais Mnangagwa aliandika katika ukurasa wake Twitter, nanukuu ” Today in Dar es Salaam, I had an excellent and productive meeting with President Magafuli, following which I engaged with, and listened to, Zimbabweans living in Tanzania. We are committed to strengthening ties with all nations for the benefit of the Zimbabwean people.”
Akimaanisha “Nimekuwa na siku nzuri sana tena yenye ufanisi mkubwa hapa DSM baada ya kukutana na Rais Magufuli na kuwasikiliza Wazimbabwe wanaoishi nchini Tanzania. Tumejidhatiti kuongeza wigo wa kushirikiana na Mataifa mengine kwa ajili ya manufaa ya watu wa Zimbabwe”
MAGAZETI LIVE: Biashara ya kushikwa nyeti, matiti yaibuka, Mateso ya korosho