Leo June 14, 2018 Bungeni Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesoma muelekeo wa hali ya uchumi kwa mwaka fedha uliopita 2017/2018 na mpango wa taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Millardayo.com nakusogezea Mambo 10 ambavyo ushuru wake umeongezeka au umepungua katika Bajeti hiyo iliyosomwa leo.
‘Ushuru wa bidhaa ya Juice iliyotengenezwa kwa matunda ambayo hayazalishwi hapa nchini utaongezeka kutoka shilingi 221 kwa lita hadi shilingi 232 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 11kwa lita’-Waziri Mpango
‘Napenda niwakumbushe tena kuwa kula fedha za miradi ya wananchi ni sawa na kula sumu’-Waziri Mpango
‘Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vifungashio vya madawa ya binadamu vitakavyotengenezwa mahsusu kwa ajili ya viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini’-Waziri Mpango
‘Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye virutubisho vinavyotumika kutengeneza vyakula vya mifugo vinavyoagizwa kutoka nje ili kupunguza gharama kwa wafugaji na kuhamasisha ufugaji bora’-Waziri Mpango
‘Ushuru wa bidhaa kwenye maji ya kunywa yasiyosindikwa kwenye chupa yaliyoagizwa kutoka nje utaongezeka kutoka shilingi 61 kwa lita hadi shilingi 64.05 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 3.05 kwa lita’-Waziri Mpango
‘Katika kipindi cha July 2017 hadi April 2018 mapato kutoka vyanzo vyote yalifikia Sh Trilioni 21.89 sawa na asilimia 69 ya lengo la mwaka la kukusanya sh Trilioni 31.71’-Waziri Mpango
‘Mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia Shilingi Trilioni 14.84 ikilinganishwa na lengo la kukusanya shilingi trilioni 19.98 kwa mwaka sawa na asilimia 74.3’-Waziri Mpango
‘Deni la Serikali limekuwa likiongezeka, hata hivyo deni hilo limeendelea kuwa himilivu na ukuaji wake unawiana na kasi ya ukuaji wa uchumi wetu’-Waziri Mpango
‘Mikataba ya ujenzi wa miundombinu inazingatia viwango vya bajeti vilivyowekwa ktk kila fungu, aidha fungu husika lisiingie mikataba nje ya viwango hivyo bila kibali cha mlipaji mkuu wa Serikali’-Waziri Mpango
‘TRA ichukue hatua za makusudi za kuboresha mahusiano kati yake na walipa kodi kwa lengo la kuondoa dhana ilojengeka miongoni mwa walipa kodi kuwa TRA inatumia nguvu na vitisho kudai kodi’-Waziri Mpango