Jeshi la Polisi katika eneo la Murang’a nchini Kenya, linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumpiga na mawe mtoto wake wa miaka mitatu na kusababisha kifo chake.
Gazeti la Daily Nation limesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia June 11 2018 katika Kijiji cha Tuthu, mwanamke huyo pia alimshambulia mama yake kwa mawe ambapo alijeruhiwa na kusadikika kuwa mwanamke huyo huenda ana matatizo ya akili.
Mashahidi katika eneo hilo wamedai kuwa mwanamke huyo alianza kurusha mawe kwa watu waliopo katika eneo hilo na kisha badae waliona mwili wa mtoto ukiwa umelala chini ndipo waliamua kuita viongozi wa eneo hilo.
Akithibitisha tukio hilo kamanda wa Polisi katika eneo hilo Ben Kipkoech amesema mtuhumiwa huyo atakabiliwa na kosa la mauji ingawa Polisi wamepata taarifa za kuwa mwanamke huyo ana matatizo ya akili lakini watahitaji ripoti ya daktari kuthibitisha.
LIVE MAGAZETI: Uchunguzi mkubwa mali za VIGOGO, Serikali kuwasaidia wenye wake wawili