Leo June 15, 2018 Mshtuko uliwakumba wakazi mji wa Kisumu nchini Kenya siku ya Alhamisi baada ya mtu aliyekuwa akijaribu kuUtoa mwili wa mtu kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi alipopigwa na kunyongwa na kundi la watu wenye hasira.
Wakazi mji huo waliamka mapema asubuhi na kukutana na mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa vipande vipande, ukiaminika kuwa ni wa msichana anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka 19 na kuwekwa kwenye begi.
Mita chache kutoka kwenye eneo hilo la kutisha ni nyumba ya mwanaume huyo ambaye ameishi kwa muda mfupi, kulikuwa na mwili mwingine ukiwa katikati ya bwawa la damu.
Watu waliojawa na hasira walimpiga mwanaume huyo hadi kifo chake.
Mtu huyo, Mike Otieno, 47 anasemekana alikuwa na mwanamke huyo aliyejulikana kama Achieng katika klabu moja ya usiku huko Kondele siku ya Jumatano usiku kabla ya kurudi naye nyumbani majira ya saa nane alfajiri.
Mashuhuda walisema mtu huyo alikuwa amenyongwa alfajiri ya Alhamisi baada ya mlinzi wa usiku walipotoa taarifa juu ya jaribio lake la kuutoa mwili wa mpenzi wake kutoka nyumbani kwake kwa kutumia begi.
“Mlinzi alisema alisikia kilio kikali cha kuomba msaada kutoka kwenye nyumba ya mwanaume huyo kabla ya vilio hivyo kumezwa na sauti kubwa ya muziki muda wa saa kumi na nusu alfajiri,” Mkuu wa Kituo Kikuu cha polisi cha Kisumu, Meshack Kiptum.
Alisema, mlinzi huyo alishtuka mnamo muda wa saa 10 alfajiri mwanaume huyo alipomwomba afungue geti ili rafiki zake waingie na kumsaidia kuhamisha mzigo muhimu.
Hata hivyo mlinzi alijawa hofu baada ya kumwona mwanaume huyo akisafisha damu ndani ya nyumba yake.
Mama mwenye nyumba, Margaret Nyarangi alisema mlinzi aliyejawa woga alimpa taarifa juu ya yale aliyoyaona.
“Mara moja nilikwenda kituo cha polisi cha Kondele kutoa taarifa na kurudi na maafisa wawili.” Mama mwenye nyumba
“Wakati polisi walipofika, alijaribu kukimbia kwa kutumia mlango wa nyuma ambapo watazamaji wachache walikusanyika lakini ndipo alipokamatwa na kupigwa hadi kifo chake,” alisema.
BREAKING: Ajali ilivyoua Askari 10 wa JKT, 25 wamejeruhiwa muda huu Mbeya
LIVE MAGAZETI: Watapigwa kipigo cha Mbwa koko!, Bajeti yang’ata yapuliza