Leo August 14, 2018 Taarifa iliyopo kuhusu hali ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla ni kuwa imezidi kuimarika ambapo jana August 13, 2018 aliweza kufanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa miguu kutoka ghorofa ya kwanza hadi ghorofa ya sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa ikiwa ni siku ya 14 sasa tangu alipopata ajali ya gari mkoani Manyara.
Waziri Kigwangalla amesema hayo wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alipomtembelea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa pole.
“Namshukuru Mungu hali yangu inazidi kuimarika jana nimefanya mazoezi nimetoka hapa nimekwenda hadi chuoni kwangu niliko soma na kurudi” amesema Waziri Kigwangalla