Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amemkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.
“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana,” -Dkt Tizeba
“Mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” -Dkt. Tizeba
Aliitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo katika awamu hii ya kwanza kuwa ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora na Geita, awamu ya pili ikijumuisha mikoa ya Singida, Kagera, na Kigoma huku awamu ya tatu ikitarajiwa kuhusisha mikoa ya Kanda ya Mashariki kwa kuzingatia ongezeko la uzalishaji wa pamba katika maeneo hayo.
Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.
Dkt Tizeba alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa Wizara ya kilimo itatekeleza mpango huo kupitia kwa Mrajis na Bodi ya Pamba ambapo kutakuwa na vituo vinane (8) vya kusimamia Trekta hizo huku kituo kimoja kikiwa ni kwa kila mkoa na viwili kwa mikoa mikubwa inayozalisha pamba kwa wingi.
Katika sherehe hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini huku Jeshi la Magereza likikabidhiwa matrekta 50 na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Matrekta 10.
“Sasa nimekunja NINJA Mbeya mpaka jeshini tutawapata” Kangi Lugola