Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Askari Mgambo, Goodluck Tarimo na Mtendaji wa Kata ya Bunju, Ibrahim Mabewa wanaokabiliwa na kesi ya
kumjeruhi kwa kutumia rungu, Robinson Oloth.
Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza Kelvin Sawala hakuachiwa kwa dhamana kwa sababu ya kushindwa kutimiza masharti.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nasoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi Hamisi Ali, kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika.
Hata hivyo baada ya Wakili Katuga kuyaeleza hayo, Wakili wa Utetezi Nassoro Mbilikira aliiomba mahakama iwapatie dhamana washtakiwa hao kwa sababu shtaka lao linadhaminika.
Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Ali amesema kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika kisheria na atakayesaini bondi ya Shilingi Laki tano.
Washtakiwa 2 walikamilisha masharti hayo, huku mshtakiwa Sawala akishindwa kutimiza masharti ambapo amerudishwa rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi October 4, mwaka huu.
Katika hati ya mashtaka washtakiwa hao wanadaiwa kumjeruhi kwa rungu Oloth ambapo walitenda kosa hilo Agosti 30 mwaka huu maeneo ya Bunju Kinondoni jijini Dar es Salaam.
BREAKING: KIVUKO CHA MV. NYERERE KIMEZAMA KIKIWA KIMESHEHENI ABIRIA