Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma anachukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonce Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Prof. Mkenda amechukua nafasi ya Mej. Jen. Mstaafu Gaudence Milanzi ambaye amestaafu.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 26 Septemba, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwao itatangazwa baadaye.