Leo July 1,2018 tunayo story kutokea Mahakama ya Wilaya ya Singida ambapo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya rushwa ya Milioni 2 inayomkabili mgombea Ubunge wa Singida Kaskazini, Haider Gulamali July 4,2018.
Awali mahakama hiyo ilisikiliza ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi,Flora Ndale.
Miongoni mwa mashahidi hao ni Ofisa Usalama mkoa wa Singida, Kiseo Nzowa anayedaiwa kupewa rushwa hiyo ambapo amedai anafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
Shahidi huyo amedai kuwa Gulamali alimpa Sh.Mil 2 ili amsaidie kupitisha jina lake kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Singida Kaskazini na kwamba yeye hakuwa Mjumbe Kamati ya Siasa Wilaya.
Amedai kuwa Gulamali alimpa fedha hizo katika bahasha huku akisema hizo ni salamu zake naye alipokea na kumpatia Meneja wa Hotel ya Urafiki Resort.
Shahidi mwingine ni Jafari Uledi ambaye ni Afisa Upelelezi Takukuru aambapo aliomba kutoa bahasha yenye Sh. milioni 2 ndani yake kama kielelezo.
Hata hivyo, upande wa utetezi walipinga kwa sababu fedha hazikutaifishwa kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha PCCB Act na Kanuni zake za 2009 yaani hakuna fomu iliyojazwa kutaifisha fedha.
Pia amedai kuwa aliyehusika kutaifisha fedha sio mtumishi wa PCCB bali ni meneja ama mlinzi wa Hotel.
Walidai hakuna karatasi iliyojazwa kwa mujibu wa Kifungu cha 38(3) CPA ili kuthibitisha kuchukua fedha na kwamba kifungu cha 169 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinakataza kupokea nyaraka ambazo zilichukuliwa kiharamu.
Kutokana na mvutano wa kisheria kuhusu kupingwa kupokelewa kwa bahasha, Mahakama iligoma kupokea bahasha yenye fedha hizo kwa kuwa haikufuata utaratibu, ambapo kesi imeahirishwa hadi July 4, 2018 ili kuendelea na usikilizwaji.
LIVE MAGAZETI: Madude yaliomng’oa Mwigulu, Watu 20 wafa kwa ajali Mbeya