Leo Jumapili July 8, 2018 saa 11:15 jioni ndege mpya ya Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kwa mara ya kwanza imetua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na Rais Magufuli.
Kila anapoongea Rais Magufuli LIVE kazi ya millardayo.com ni kukusogezea NUKUU muhimu katika hotuba hiyo. Leo July 8, 2018 nakusogezea MAMBO 7 kutoka katika mapokezi ya DREAMLINER.
Jambo la Kwanza ni kauli ya “Watapata tabu sana”>>> “Nina imani kubwa kuwa watanzania wamefurahi ujio wa ndege yetu hii kama wapo ambao hawajafurahi basi watapata tabu sana”- Rais Magufuli
Jambo la Pili ni kufufua Shirika la ATCL “Tumefufua ATCL kurejesha heshima ya nchi, ilikuwa aibu kutokuwa na ndege kwa nchi kubwa kama Tanzania yenye sifa mbalimbali – Rais Magufuli
Jambo la Tatu ni msisitizo wa kulipa kodi “Ndege hizi ni matokeo ya Watanzania kulipa kodi na kuchapakazi. Nawapongeza wote walioshiriki kikamilifu, Ndege zote hizi tumenunua kwa fedha zetu wenyewe, hatujakopa kwa mtu” – Rais Magufuli
Jambo la Nne ni salamu “Tunataka Balozi wa Marekani utufikishie salam Boeing kuwa ile Dreamliner ya pili waikamilishe haraka, hela tunazo” – Rais Magufuli
Jambo la Tano ni kuongeza Mapato “Tumeleta ndege hizi pia ili ziimarishe na kuongeza mapato yetu ya utalii nchini, 70% ya watalii wanatumia ndege” Rais Magufuli
Jambo la Sita ni kuboresha huduma “Tunaboresha usafiri wa reli, majini na barabara, waliodhani kuwa maboresho ya Bandari hayana tija sasa wameaibika, tunatekeleza kwa kasi miradi ya maji, umeme, Afya na Elimu, mwaka huu tutaanza mradi wa umeme wa Stiglers” -Rais Magufuli.
Jambo la Saba la mwisho ni “Tumebana mianya yote na tunahakikisha kuwa kila hela inayopatikana inatumika kwa maslahi ya watanzania, Tanzania yenye maendeleo, Tanzania yenye sifa, Tanzania yenye neema inakuja, tumefanikiwa hili tutafanikiwa na mengine.” Rais Magufuli