Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na wananchi wote waliompa pole na waliojitokeza kumfariji wakati wa msiba wa Dada yake Monica Joseph Magufuli aliyefariki dunia tarehe 19 Agosti.
Rais Magufuli amesema upendo na ushirikiano ambao umeoneshwa na kila aliyeguswa na kifo cha Dada yake umemfariji kwa kiasi kikubwa yeye na familia nzima, na umewatia nguvu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi.
“Kifo cha Dada yangu Monica, kimesababisha huzuni na majonzi makubwa kwetu sisi wanafamilia kwa kuwa tulimtegemea kwa mengi na ndiye alikuwa akimlea Mama yetu Bibi Suzana Ngolo Magufuli,” -Rais Magufuli
“Lakini salamu za pole, maombi yenu na tulipowaona wengi mmekuja kuungana nasi kumsindikiza katika safari ya mwisho, tumefarijika sana na tumepata nguvu.” Rais Magufuli
“Kwa niaba ya familia naomba kuwashukuru sana nyote kwa moyo wenu wa upendo na maombi yenu, naamini mtaendelea kuungana nasi kumuombea Dada yetu Monica apumzike mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Magufuli katika shukrani hizo.
RC Mbeya chimbo la Waathirika Dawa za Kulevya amtaja RAY C “haina noma endeleeni”