Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameuvunja uongozi wa soko la Sido Jijini hapo kufuatia kuwepo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zikiwemo milioni 15 zilizochangishwa kwa ajili ya rambirambi ya kifo cha Mbunge, marehemu Leonidas Gama.
Mbali na Milioni 15 za rambirambi, pia wanatuhumiwa kutafuna kiasi cha shilingi Milioni 10 zilitolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati soko hilo lililopoteketea kwa moto Agosti 2017.
Katika hatua nyingine mkuu huyo, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, James Kasusura kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanapata leseni za biashara sambamba na namba ya mlipa kodi ili waweze kutambulika.
Mwimbaji wa Gospel afurahia nyimbo zake kupigwa Disco, asema Bongofleva haimsaidii