Leo August 7, 2018 Muungano wa taasisi yaa uhifadhi wa mazingira duniani (WWF Tanzania) na taasisi CARE Inernational, wameendesha mafunzo ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa wakulima na wafugaji, uongezaji tija katika kilimo, ujumishwaji wa wanawake, vijana, na kuondoa umasikini – katika sherehe ya wakulima ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8/8.
Mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuwapatia wakulima elimu ya uwekezaji rafiki wa mazingira kwa maendeleo endelevu katika ukanda wa SAGCOT yalifanyika katika banda la SAGCOT katika viwanja vya John Mwakangale, mkoani Mbeya leo August 7.
Akiongea katika semina hiyo, Makfura Evergris, Mwangalizi wa mradi wa CARE-WWF Alliance ofisi ya Iringa amesema “Wakulima wanapaswa kuelewa umuhimu wa kilimo hifadhi ambacho kitaleta kilimo endelevu kwa ajili ya kuinua maisha yao kiuchumi na kuleta tija katika uchumi wa viwanda hapa nchini.”
Aidha; amesema kuna umuhimu mkubwa wa wakulima kupewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji ili kufanikisha adhma hii. Pia alisisitiza umuhimu wa wadau wa mazingira na kilimo kufanya kazi kwa pamoja katika kutoa mafunzo na kusambaza elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na shughuli za kibinadamu kufanyika kwa uangalifu mkubwa wa kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwa vizazi vya sasa na baadae.
Makfura, akitoa mfano katika Kongani ya Ihemi na Mbarali, amesema kuwa wakulima katika eneo hili wanapaswa kuelewa kuwa shughuli zao za kilimo zinaweza kuwa na madhara hasi ama chanya katika mtiririko wa mto Ruaha Mkuu (The great Ruaha River) ambao unatiririsha maji yake kupitia hifadhi ya Ruaha (Ruaha National Park – RUNAPA) ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote Afrika mashariki na kati.
Akisisitiza umuhimu wa kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ambayo itawezesha kuainisha maeneo mbalimbali kwaajili ya matumizi ya ardhi katika ngazi ya kijiji hadi wilaya.
“ Mradi wa CARE-WWF Alliance unaamini kwamba ni kwa njia ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ndio itaziwezesha jamii za wakulima na wafugaji kuondokana na umaskini kupitia shughuli zao wanazozifanya, huku wakizingatia uhifadhi wa mazingira yanayowazunguka” Makfura
“Akitolea mfano mpango wa matumizi bora ya ardhi ulifanyika katika vijiji 6 vya wilaya ya Mufindi, vijiji vya Lugodalutali, Igombavanu, Utosi, Mapogoro, Uhambila na Kibada.” Makfura
Kwa upande wa mradi wa uwekezaji endelevu wa shirika la uhifadhi wa mazingira duniani WWF Tanzania, Afisa mradi, Happynes Minja, alisisitiza juu ya utunzaji wa mazingira kwa wakulima wadogo wadogo na kwa wawekezaji walioko katika sekta ya kilimo na ufugaji ili kuhakikisha uwekezaji wao unakuwa na tija.
Nae Beno Mgayo, ambaye ni moja ya washiriki aliyewakilisha kikundi cha Lusitu Agribusiness group kutoka mkoani Njombe, amepongeza kazi nzuri zinazofanywa na WWF Tanzania huku akikisisitiza kuongezwa kwa nguvu kubwa katika udhamini wa upandaji wa miti rafiki wa maingira katika kutunza vyanzo vya maji mkoani humo.
Sherehe hizi za waklima kwa mwaka huu 2018 zinabeba Kauli mbiu ya “Kuwekeza katika kilimo, ufugaji na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda.”
‘Wazee wa ile hela tuma kwa namba hii’ kuyaingiza Makampuni ya simu matatani
https://youtu.be/jJiGL7WT-p4