Leo May 26, 2018 Serikali imetangaza mikakati mipya iliyopangwa kuokoa hifadhi la ziwa la Manyara, ambalo linatishiwa kupotea kwa sababu ya shughuli za kilimo.
Telesia Mahonga, Kamishna wa Wilaya ya Karatu, amesema kuwa mazingira ya Ziwa Manyara yako chini ya tishio kubwa la kupotea na kama haitatunzwa vizuri, hifadhi hiyo ya kaskazini mwa Tanzania itatoweka.
“Tumewasii wakulima wa upande sehemu za juu ya mito kuhama, na ikiwa wanakataa amri hiyo, tutawafukuza kwa nguvu,” amesema afisa huyo, akielezea Hifadhi hiyo kuwa muhimu kwa flamingos ambazo ziko katika ziwa.
Hifadhi hiyo ni makazi ya zaidi ya aina 400 za ndege.