Mkoani Kigoma kuna udongo maarufu unaojulikana kwa jina la udongo wa pemba, Husna Kabezi ni mjasiriamali aishie Kigoma ambae aliacha kufanya kazi za ndani mkoani Tabora mwaka 1999 kwa sababu ya manyanyaso na kuamua kuanza kazi za kufinyanga udogo ambao unapendwa sana kutumiwa na wanawake wajawazito.
Kwa miaka mingi Husna ameifanya kazi hiyo inamuingizia kipato pamoja na wanawake wengine Mkoani Kigoma huku yeye akisomesha watoto kupitia kazi hiyo.
AyoTv na millardayo.com alifika katika sehemu anayofanyia kazi na kuweza kuzungumza nae kwa undani zaidi juu ya kazi yake mafanikio yake na changamoto zake.