Leo December 13, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara, Ikulu Jijini DSM.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Huruma Mkuchika na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardius Kilangi, Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere.
HUYU NDIE IBRAHIM PASHA WA TAMTHILIA SULTAN LEO NI BIRTHADY YAKE